Jumanne 23 Desemba 2025 - 14:24
Mwenendo wa Mazungumzo na Israel ni hatari kubwa kwa Lebanon

Hawza/ Ali Fayyadh ameonesha wasiwasi wake mkubwa kuhusu maendeleo ya mazungumzo ya Lebanon na Israel, akisema kuwa; kwa kuteleza Lebanon kuelekea kufanya mazungumzo na Waisraeli chini ya uongozi wa shakhsia zisizokuwa za kijeshi, mwelekeo huu umeingia katika hatari na tahadhari nzito inayotia wasiwasi mkubwa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hizbullah iliandaa hafla kubwa ya kumbukumbu ya shahidi Ali al-Hadi Ghassan Hajjazi (Abu Ali) katika mji wa Tayr Debba. Hafla hiyo ilifanyika kwa ushiriki wa Ali Fayyad, mjumbe wa kikundi cha “Uaminifu kwa Muqawama”.

Ali Fayyadh, katika hotuba yake kwenye hafla hiyo, alieleza wasiwasi wake kuhusu mwenendo wa mazungumzo kati ya Lebanon na Israel, akisema: “Kwa kuteleza Lebanon kuelekea kwenye mazungumzo na Waisraeli chini ya uongozi usionkuwa wa kijeshi, mwelekeo huu umejikuta ukikabiliwa na hatari na tahadhari nzito zinazotia wasiwasi mkubwa.”

Aliongeza kuwa; misimamo iliyotolewa na Marekani na Israel katika kuitikia kikao cha hivi karibuni kilichofanyika Naqoura, inaashiria wazi kuwepo kwa mijadala kuhusu ushirikiano wa kiuchumi na kijeshi kati ya Lebanon na adui Muisraeli, pamoja na kusukumwa mbele kwa miradi ya kiuchumi. Mazungumzo haya yameunganisha mkondo wa kiusalama na mkondo wa kisiasa, na kuyachukulia maendeleo katika nyanja hizi mbili kwa mtazamo wa pamoja na uliounganishwa.

Mjumbe huyu wa kikundi cha Uaminifu kwa Muqawama, huku akisisitiza kwamba kuigeuza kamati ya utaratibu (mechanism committee) kuwa jukwaa la kujadili masuala haya ni kupotoka na hatari kuhusu Azimio la Kimataifa Na. 1701 pamoja na makubaliano ya kusitisha mapigano ya tarehe 27 Novemba 2024, alisema: “Hatua hii inaipeleka Lebanon kuelekea kwenye shimo la hatari, ambalo matokeo yake ya maafa hayaepukiki, na inaweka mchakato wa mazungumzo ndani ya masharti na matakwa ya Israel, hali ambayo kujinasua kutoka ndani yake itakuwa vigumu sana.”

Aliendelea kuonya kwamba; kujizuia kwa Lebanon kujadili, ndani ya kamati ya utaratibu, masuala ya kuondoka kwa Israel kutoka maeneo yanayokaliwa kimabavu, kusitishwa kwa vitendo vya uhasama, pamoja na kuachiliwa huru wafungwa wa Lebanon, na badala yake kushughulikia masuala mengine ya kiuchumi au kisiasa, ni jambo hatari mno.

Nguzo thabiti za msimamo wa Lebanon katika mazungumzo

Ali Fayyadh alisisitiza kwamba; kurejea bila masharti kwa wakazi wa vijiji vya mpakani, mamlaka kamili ya dola juu ya ardhi yote ya Lebanon, kupelekwa Jeshi la Lebanon katika maeneo yote hususan maeneo ya mpakani, pamoja na haki ya Lebanon ya kujilinda na kumiliki nyenzo zitakazowezesha utekelezaji wa haki hiyo, ni lazima viwe nguzo katika msimamo wa Lebanon kwenye mazungumzo, ambazo hairuhusiwi kabisa kuziacha.

Mwisho, alionya kwamba; kujisalimisha kwa Lebanon katika mazungumzo, wakati Israel ikiendelea kila siku kufanya mauaji na mashambulizi ya anga yanayoharibu maisha na riziki za raia wa Lebanon, kunazalisha udhaifu hatari sana katika msimamo wa mazungumzo wa Lebanon, na kunadhihirisha utoaji wa upendeleo wa bure kwa adui.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha